Michezo

Mtu wangu wa nguvu ninayo ripoti kutoka Uturuki waliko weka kambi Taifa Stars (+Audio)

on

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars bado ipo nchini Uturuki inaendelea na kambi yake ya siku nane kujiandaa kabla kucheza mechi dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles ya kuwania kufuzu AFCON 2017, mchezo utakaopigwa Septemba 5 katika Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.

ball

August 27 kocha wa Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa ametoa ripoti kuhusu maendeleo ya kambi hiyo sambamba na hali za wachezaji, Mkwasa amethibitisha wachezaji kuwa katika hali nzuri kasoro Abdi Banda ndio anasumbuliwa na misuli. Vipi kuhusu uamuzi wa kuweka kambi Uturuki ikiwa kuna hali ya hewa ya baridi ukilinganisha na sehemu utakapopigwa mchezo huo.

DSC_0030

“Kwa ujumla kambi inaenda vizuri wachezaji wapo vizuri kasoro Abdi Banda ndio amepata matatizo ya misuli, tupo huku kwa kambi tunajua kuna baridi ila sehemu yenye baridi kuna Oxygen ndogo hivyo mapafu yanafanya kazi sana kutafuta hewa hivyo ukizoea kuvuta hewa kidogo ukija katika sehemu ambayo ina hewa nyingi inakuwa rahisi kucheza vizuri”>>> Mkwasa

Taifa Stars itacheza mechi ya kirafiki na timu ya taifa ya Libya siku ya August 28 ikiwa Uturuki kama sehemu ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Nigeria.

Hii ni sauti ya Mkwasa

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

[/tps_header]

Tupia Comments