Raia wa Marekani Terry Sutherland ambaye ni Mlemavu wa macho ameibua mjadala baada ya kupata kibali cha kumiliki bunduki licha ya hali yake ya upofu.
Sutherland ambaye anatumia fimbo maalum ya mtembezi aliweza kufuata mchakato wote wa maombi ya kibali cha kumiliki silaha kwa siri jambo ambalo limezua maswali kuhusu sheria za udhibiti wa silaha Nchini Marekani
Aidha Mlemavu huyo wa macho alieleza kuwa aliweza kumaliza mchakato wote wa maombi kwa urahisi na hakukuwa na kizuizi chochote katika kupata kibali hicho.
Kufuatia hatua hiyo mjadala kuhusu sheria za silaha umeongezeka Nchini humo huku Wanasiasa na Wafuasi wa sheria za silaha wakijadili iwapo mchakato wa kutoa leseni unahitaji kurekebishwa ili kuhakikisha usalama wa umma, wakati huo huo baadhi Wanakosoa hatua ya mlemavu huyo huku wengine wakitetea haki ya kumiliki silaha kwa Watu wote bila kujali hali ya kiafya.