AyoTV

‘Wale Wasanii waliowekwa ndani haikua vita dhidi ya dawa za kulevya’- Mbunge Mlinga

on

Kutoka Bungeni Dodoma Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga ni miongoni mwa waliopata nafasi ya kusimama kwenye kuhitimisha Mkutano wa sita wa Bunge na kuhoji uhalali wa baadhi ya Watuhumiwa wa dawa za kulevya kutajwa majina yao kupitia vyombo vya habari.

Mlinga amesema “Sipingi vita dhidi ya dawa za kulevya ila ninacholaani ni mtu kutumia madaraka yake kupigana vita binafsi kuigeuza kuwa vita ya kitaifa, niko tayari kusimama mbele ya Rais kumwambia chanzo cha vita hii

Vita haijaanza kwa ajili ya dawa za kulevya, imeanza kwa ugomvi binafsi baada ya kuona ita back-fire wakaigeuza kuwa vita ya dawa za kulevya, wale Wasanii waliowekwa ndani ilikua nini?” – Mlinga

Mtazame Mbunge Mlinga zaidi kwenye hii video hapa chini

VIDEO: Unapotangaza Mtu aje Polisi saa 5, wewe ni nani? – FREEMAN MBOWE…… tazama zaidi kwenye hii video hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments