Baada ya sauti iliyokuwa inasambaa mitandaoni ikihusisha sauti ya Mwigizaji Steve Nyerere na mama wa mwigizaji Wema Sepetu ambapo Steve Nyerere kwenye sauti hiyo alidai kuwa alishawishi baadhi ya wabunge kuzungumzia ishu ya dawa za kulevya bungeni lakini hata hivyo Steve alijitokeza mbele ya wanahabari na kudai hakuwahi kuwashawishi wabunge.
AyoTV na millardayo.com imempata mbunge wa jimbo la Ulanga Goodluck Mlinga ambaye alikuwa mmoja wa wabunge ambao walichangia katika sakata la dawa za kulevya bungeni na hapa amejibu kama aliwahi kushawishiwa na Steve Nyerere kufanya hivyo.
“Mazingira ndio yalisababisha aseme vile lakini mimi sikuwahi kuonana nae ila baadae alikuja kutoa shukrani kwa wabunge kuongelea lile suala na hata baada ya sauti nilitaka kumpeleka mahakamni lakini aliwahi kuomba radhi”-Mbunge Mlinga
FULL VIDEO: Steve Nyerere alivyotokwa machozi na kuongelea simu ya Mama Wema, Bonyeza play hapa chini