Mkurugenzi wa Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa (CDC) cha nchini Marekani, Robert Redfield amesema kuna uwezekano mlipuko wa pili wa COVID 19 ukatokea msimu wa baridi, wakati wa kipindi cha mafua.
Kauli yake inakuja baada ya Magavana kadhaa kulegeza masharti yaliyowekwa kudhibiti maambukizi ya Corona Virus ili kufungua uchumi katika majimbo yao licha ya ongezeko kubwa la waathirika.
Amesema, mlipuko wa pili unaweza kuwa na athari kubwa zaidi kuliko hali ilivyo hivi sasa kwani nchi hiyo itakuwa inakabiliwa na magonjwa mawili kwa wakati mmoja. Marekani imerekodi visa 819,164, vifo 45,340 na waliopona 82,973 hadi kufikia asubuhi ya leo.
MAPAMBANO DHIDI YA CORONA: VYOMBO VYA HABARI 10 VYAPEWA SANITIZER