Top Stories

Mlipuko wa homa ya Uti wa Mgongo waua watu 129, Serikali yatoa tamko

on

Serikali ya Tanzania imesema kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika kupitia mitandao kumejitokeza mlipuko wa ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, Jimbo la Tshopo ambapo Watu 261 wameugua na 129 kufariki.

Wizara ya Afya Tanzania imewataka Watanzania kuchukua tahadhari kwani magonjwa hayana mipaka hususani mikoa inayopakana na DRC.

Dalili kuu za ugonjwa huu ni homa kali, kichwa kuuma, kutapika, kuogopa mwanga, kuchanganyikiwa na shingo kukakamaa ———> “ugonjwa huu unaweza kusababisha madhara makubwa kwenye ubongo, kupotea kwa usikivu au ulemavu mwingine wa kudumu na hata kupoteza maisha”

Ugonjwa huu husababishwa na vinkers aina ya bakteria wanaojulikana kama Neisseria Meningitids na huambukizwa kutoka Mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya hewa au kukaa na Mtu mwenye maambukizi na huchukua siku 2 hadi 10 tangu kuambukizwa hadi kuanza kuonesha dalili ———“Watu wanapaswa kuepuka mikusanyiko na Watu wengi”

AJABU LA DUNIA, MAMA AJIFUNGUA KALUNGUYEYE “NIMESIKIA UCHUNGU, KIMETOKA NA DAMU KAMA UZAZI ULIVYO”

Tupia Comments