Watu 12 wamefariki kwa ugonjwa wa kipindupindu na 95 wametembelea hospitali zenye dalili zinazoashiria kuwa wanaweza kuwa na ugonjwa huo huko Tshwane, manispaa inayojumuisha mji mkuu wa Afrika Kusini wa Pretoria.
Idara ya afya katika jimbo la Afrika Kusini la Gauteng Jumapili ilitangaza visa vipya 19 vya Kipindupindu ikiwa ni pamoja na vifo 10, katika mji wa Hamman-skraal.
kesi 19 za kipindupindu, pamoja na wale waliokufa, zilithibitishwa na 37 wamelazwa hospitalini, idara ya afya ya mkoa ilisema katika taarifa. Sehemu kuu ya mlipuko huo iko Hammanskraal kaskazini
Afrika Kusini iliripoti kifo chake cha kwanza kutokana na kipindupindu mwezi Februari mwaka huu baada ya wagonjwa waliokuwa na virusi hivyo, kuwasili kutoka nchini Malawi.
Haikubainika wazi ni wagonjwa wangapi wa kipindupindu walioko nchini kote lakini jimbo hilo lenye watu wengi zaidi la Gauteng, ambako Johannesburg na Pretoria zinapatikana, ndilo lililoathirika zaidi.
Mlipuko wa mwisho nchini Afrika Kusini ulishuhudiwa kati ya mwaka 2008 na 2009, wakati ambapo, takriban visa 12,000 viliripotiwa, kufuatia mlipuko katika nchi jirani ya Zimbabwe.
Hali hiyo inaelezwa kusababisha ongezeko la wagonjwa waliokuwa wametoka nchi za nje, na maambukizi ya ndani.
chanzo:VOA