Visa vya virusi vya polio vinavyotokana na aina ya 2 (cVDPV2) vimegunduliwa kwa mtoto wa miaka minne kutoka wilaya ya Isalé, magharibi mwa Burundi, ambaye hakuwa amechanjwa dhidi ya ugonjwa wa polio, pamoja na watoto wengine wawili ambao walitangamana na mvulana huyo wa miaka minne,WHO imesema katika taarifa.
Sampuli tano kutoka kwa idara ya ukaguzi wa mazingira ya maji machafu pia zimethibitisha uwepo wa virusi vya polio, taarifa hiyo imebainisha.
Kwa mujibu wa WHO, serikali ya Burundi, ambayo imetangaza kugunduliwa kwa virusi hivyo kama “dharura ya kitaifa ya afya ya umma”, inapanga kuanzisha kampeni ya chanjo ya polio ili kuwalinda watoto wote wenye umri wa miaka 0-7 dhidi ya virusi hivyo.
“Polio inaambukiza sana na ni muhimu kuchukua hatua haraka ili kuwalinda watoto kupitia chanjo inayofaa,” amesema Dk Matshidiso Moeti, Mkurugenzi wa WHO katika kanda ya Afrika.
Afisa huyo anasema shirika lake linaunga mkono
juhudi za kitaifa za kuongeza chanjo ya polio ili kuhakikiha kwama hakuna mtoto anayeachwa nyuma na hatari ya athari za ugonjwa huo.
Kulingana na WHO, kuzunguka kwa virusi vya polio aina ya 2 ndio aina ya kawaida ya polio barani Afrika na milipuko ya aina hii ya virusi vya polio ndio inayotokea zaidi na zaidi ya kesi 400 za kupooza kwa papo hapo kuripotiwa katika nchi 14 zilizoathirika mwaka 2022.