Breaking News

UPDATES: Uokoaji unaendelea kutafuta waliopotea baada ya Meli kuzama Ziwa Victoria ikiwa na watu 25

on

Baada ya ajali ya Ndege kuua watu 11 jana Ngorongoro Arusha, taarifa nyingine za usiku wa kuamkia leo ni kuhusu Meli iliyozama Ziwa Victoria ikitokea Kagera kuelekea Mwanza ikiwa na watu 25.

Mkuu wa Wilaya ya Muleba Richard Luyango ameongea na AyoTV na millardayo.com na kusema “Ni Meli ndogo ikiwa na mizigo na watu 25 wakiwemo Manahodha 6, Abiria wenye mizigo yao wanne, Wafanyakazi vibarua 15 ambapo upepo mkali ulipozidi ikapinduka”

“Ilipinduka karibu na Kitongoji cha Kakomakoma walihitaji msaada  na watu wakaenda usiku huohuo wakaokoa watu 22 isipokua watu watatu hawajaonekana mpaka sasa hivi, hao 22 waliookolewa wako salama”

Unaweza kumsikiliza zaidi Mkuu wa Wilaya akiongea hapa chini

VIDEO: AJALI YA TRENI TANZANIA IKITOKEA KIGOMA-DSM… BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUITAZAMA

VIDEO: “HILI NI TATIZO LAZIMA TUJUE TUNAKWENDA WAPI” – HUSSEIN BASHE ASEMA LEO BUNGENI, MTAZAME ZAIDI HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments