Duniani

Dakika 4 za kuenjoy ngoma ya bendi ya wafungwa Malawi waliotajwa Tuzo za Grammy.. (+Video)

on

Kama ulikuwa karibu na radio yako jana December 16 2015 moja ya stori kubwa iliyosikika kwenye AMPLIFAYA ilikuwa ni hii inayohusu bendi ya wafungwa kutoka Malawi iliyotajwa kuingia kwenye Tuzo za Grammy zitakazotolewa February 2016.

Bendi Inaitwa Zomba Prison Band na tayari wana album ambayo wameipa jina la ‘I Have No Everything Here‘, bendi hiyo ina timu ya watu 16 ambao wote ni wafungwa ambao wengi wao wanatumikia kifungo cha maisha.

Tuzo hizo zitatolewa February 2016 japo mpaka sasa haijathibitishwa kama wafungwa hao wataruhusiwa kwenda kushiriki utoaji wa Tuzo hizo Marekani.

Hii hapa moja ya ngoma zao mtu wangu, Zomba Prison Project  ‘Please Don’t Kill My Child’

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments