Premier Bet
TMDA Ad

Top Stories

Majambazi wawili na Raia wawili wauawa Kigoma “Tumewatendea haki tumewawahi” (+video)

on

Leo July 16, 2019 Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma limethibitsha kuuawa kwa Wananchi wawili pamoja na Majambazi wawili katika mapambano ya kurushiana Risasi baina ya Polisi na majambazi katika Kijiji cha Kumtundu Kata ya Makere Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma ACP Martin Otieno ameeleza kuwa tukio hilo ni mwendelezo wa operehseni maalumu ya kutokomeza ujumbazi Mkoani humo ambapo licha ya kuuawa kwa majambazi wawili wengine kati yao walikimbia na silaha.

ACP Martini Otieno ameeleza kuwa baada ya kupata taarifa za ndani kutoka kwa wakazi wa maeneo hayo zinazoelezea eneo ambalo majambazi hao huweka makazi yao ndipo Polisi wakiwa pamoja na wananchi kadhaa majira ya saa 3 usiku wa kuamikia leo waliwavamia majambazi hao katika maeneo yao ya kujificha.

MCHINA KAKUTANA NA MOTO WA MAGUFULI SITE “NAKUONYA WEWE”

Soma na hizi

Tupia Comments