Leo January 24, 2019 Rais wa DR Congo Felix Tshisekedi ameugua ghafla wakati akitoa hotuba muda mfupi baada ya kuapishwa katika hafla iliyohudhuriwa na Rais Mstaafu Kabila.
Rais Tshisekedi baada ya kuapishwa alitoa hotuba kwa wananchi lakini alishindwa kuendelea na kusema kwamba anajisikia vibaya na hawezi kuendelea kuongea.
“Sijisikii vizuri, sijisikii vizuri kabisa “ ni maneno ya Rais Tshisekedi na akaacha kuendelea kuhutubia taifa
Akitoa hotuba amesema atahakikisha anasimamia Demokrasia na amani DRC ambayo imepotea kwa muda mrefu.
MAMA ALIYESOMESHA MWANAE ULAYA KWA KUUZA MBOGA AKIPIGA PUSH-UP