Top Stories

Mambo matano aliyoyasema JPM Bandarini ikiwemo kupandisha cheo

on

Leo May 15, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza bandari ya Dar es salaam na kukagua matanki ya mafuta ya kupikia.

Nakusogezea MAMBO MATANO aliyoyasema JPM Bandarini ikiwemo kumpandisha cheo aliyekuwa Kaimu Kamishna TRA Bandari ya DSM Ben Usaje kuwa Kamishna kamili TRA bandarini hapo baada ya kusimamia vyema uchunguzi alioagiza ufanyike bandarini.

Rais Magufuli amebaini kuwa baadhi ya makontena yaliyodaiwa kuwa na mafuta ghafi (mafuta ya kupikia) yalikuwa na mafuta masafi.

Rais Magufuli amesema “Wafanyabiashara wanaotumia nafasi zao kulaghai watu, huwa mnawasikia kwenye vyombo vya habari wanasema mwaka huu mafuta yamepanda bei, nawaomba tuwe wazalendo. ‘Crude Oil’ ichajiwe bei ya juu ili kuimarisha viwanda vya ndani.”

Kingine nilichonukuu katika ziara ya JPM ni maagizo kwa Mkemia Mkuu “Mkemia Mkuu nataka sampo zozote mtakazokuwa mnapewa fanyeni kwa utaratibu kwa kuzingatia maadili, mkiletewa mkono wa albino semeni mkono wa albino msije sema wa mbwa. Mkiletewa dawa ya kulevya semeni haya ni madawa ya kulevya sio unga wa muhogo”

Hitimisho lilikuwa ni hii kauli “Hakuna tatizo la mafuta isipokuwa baadhi ya wafanyabiashara wachache wasio waaminifu wameitengeneza hali hiyo”

BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA HAYO YOTE AKIWA KATIKA BANDARI YA DSM

Soma na hizi

Tupia Comments