Top Stories

Zitto Kabwe ameandika Twitter “Nimetishiwa kuuawa nikiwa Bungeni”

on

Leo January 18, 2019 Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amedai kuwa ametishiwa kuuawa akiwa Bungeni Dodoma kupitia akaunti yake ya Twitter amedai kutishiwa na Mtu aliyemtaja kama Afisa Usalama wa Taifa.

Nazinukuu Tweet za Zitto Kabwe kama zilivyoandikwa Twitter “Leo mchana nimetishiwa kuuwawa na Afisa Usalama wa Taifa hapa Bungeni ukumbi wa Msekwa mara baada ya Mwenyekiti wa Kamati kuniondoa kikaoni kwa kuwa sio mjumbe ( kinyume na kanuni za Bunge ). Afisa huyo alinifuata nje na kuniambia ‘ dawa yako wewe ni kukuua”

Hakika nilikasirika sana na nikamwambia yeye na hao waliomtuma ni wapumbavu watakufa wao kwanza. Kama si Mbunge David Silinde kutokea ninaamini jambo baya lingetokea. Nimeandika Barua kwa Spika kutoa malalamiko rasmi ya Tabia za watumishi wa TISS kuwatisha Wabunge” Zitto Kabwe 

Serikali imejaza maafisa wa TISS hapa Bungeni kutisha Wabunge wasiwe huru kufanya kazi zao. Nimeambiwa kuwa mbunge Zubby Sakuru pia kakumbana na kadhia hii ya kutishwa ndani ya ukumbi Kamati Zikiendelea. Bunge la Wananchi limetiwa mfukoni na Serikali ( executive)” Zitto Kabwe

RC Mwanri kambana Injinia site “Usilete njaa, mito inahama kama stuli”

 

Soma na hizi

Tupia Comments