Top Stories

Wanandoa waiba mtoto Hospitalini Mbeya

on

Wanandoa Happy Charles na Chiluba Peter ambaye ni dereva wa teksi anayeegesha eneo la Hospitali ya Mkoa wa Mbeya wanashikiliwa na Polisi wakituhumiwa kuhusika na wizi mtoto wa kike.

February 1, 2018 mwanamke aliyejifanya muuguzi wa Hospitali hiyo aliingia katika wodi ya wazazi na kumchukua mtoto wa Sarah Mwasanga kwa madai ya kwenda kumpatia chanjo.

Akizungumza na waandishi wa habari February 3, 2018 Kaimu Mganga Mkuu wa Hosptali hiyo, Yahaya Msuya amesema mara baada ya tukio hilo mama wa mtoto huyo alitoa taarifa kwa uongozi wa hospitali na uongozi wa hosptali kwa kushirikiana na polisi na wananchi waliweka mitego katika maeneo mbalimbali iliyowezesha mtoto huyo kupatikana akiwa hai.

Amesema hali ya mtoto huyo inaendelea vizuri na yupo katika uangalizi wa madaktari kutokana na
mazingira waliyomkuta baada ya kuibwa.

Namnukuu Mama wa mtoto huyo, “Siamini kilichotokea, nilitambua mwanagu amechukuliwa kimazingira na mwanamke aliyefika katika wodi ya wazazi akiwa kama muuguzi kwa kweli yote namwachia Mungu.”

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohamed Mpinga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mpaka sasa wanawashikiliwa wanandoa hao.

Amesema bado wanaendelea na taratibu za kisheria za kuwahoji na watafikishwa mahakamani wakati wowote mara baada ya uchunguzi kukamilika.

“HUU NI UHUJUMU UCHUMI, WOTE TUTAWACHUKULIA HATUA” -NAIBU WAZIRI MWANJELWA

Soma na hizi

Tupia Comments