Leo May 11, 2018 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amezindua Operesheni Nzagamba itakayozuia utoroshwaji mifugo nje ya nchi, kuingiza madawa zenye madhara ikiwemo kuzuia chakula cha mifugo ambacho hakiruhusiwi.
Waziri Mpina amewagomea wananchi wanaofanya mnada wa mifugo katika wilaya Longido iliyopo mpakani mwa Tanzania na Kenya waliotaka kupunguza kodi ya Shilingi 5000 kwa mbuzi mmoja pamoja na 20000 kwa ng’ombe akidai kwamba wananchi walipe kodi kwa kuwa kuna kiwanda kinajengwa eneo hilo kitakachosaidia eneo hilo.