Michezo

Samuel Eto’o akacha kuingia katika siasa

on

Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon Samuel Eto’o katika mahojiano yake na AFP aliulizwa kuwa ana mpango wa kuingia katika siasa kama inavyoripotiwa kuwa anashinikizwa na baadhi ya watu kufanya hivyo, Eto’o amekanusha kuwa hana mpango huo.

“Kila mmoja amezaliwa na nyota yake ya ushindi kila mmoja kuna wakati alijihusisha na siasa katika level yake kwa wakati fulani, ila mimi hainivutii kila mmoja anataka mimi niingingie huko (siasa) ni wazo ninalo lakini nimewajibu halipo katika mpango wangu kwa sasa”>>> Eto’o

“Kila raia ana haki ya kugombea kama atataka lakini katika nchi yangu nahisi hizo ni nafasi ambazo zimetengwa kwa ajili ya watu maalum, binafsi hayo sio malengo yangu”>>> Eto’o

Hilo limezuka ikiwa kuna kuwepo na ongezeko la wachezaji wa zamani kutaka kuingia kwenye siasa, Rais wa sasa wa Liberia George Weah aliwahi kuwa mwanasoka wa kiwango cha juu, mkenya Mc Donald Mariga anagombea Ubunge wa Kibra November 7 wakati Didier Drogba anahusishwa kutaka kugombea Urais wa shirikisho la soka Ivory Coast (IFF).

AUDIO: Edo Kumwembe aeleza kocha anaestahili kuwa Yanga sio Zahera

Soma na hizi

Tupia Comments