Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa Nchini Tanzania (MSD), Laurean Bwanakunu ,amesema elimu ya sasa siyo karatasi bali ni vitendo utakavyo kufanya maofisini baada ya kupata mafunzo uliyopata darasani.
Ameyasema hayo Disemba 13, 2019 alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya Chuo cha Uhasibu (IAA) tawi la Dar es Salaam, ambapo amesema baada ya kuhitimu mafunzo, lazima ujifunze kuwa tofauti katika utendaji wako ili kile unachokifanya kionekane na kujulikana kama wewe ndiyo umefanya kazi hiyo.
“ Muhitimu mzuri ni yule anayejua kuwa tofauti na wenzake kiutendaji na kuwa tofauti na wenzako ili muhajiri wako aweze kuona utofauti wako na kuanza kukufuatilia, “amesema Bwanakunu.
Aidha kwa upande wa wahitimu kutoka chuo hicho wamesema baada ya kumaliza mafunzo yao wanaenda kuonyesha utofauti kiutendaje kazi ili waweze kufikia malengo ambayo hata serikali itatambua uwepo wao baada ya kupata elimu.
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi waliohitimu Esther Kilongola alikishukuru chuo kwa kuwawezesha kumaliza kwa wakati huku akisifu Chuo kwa umahiri wake katika ufundishaji na kuahidi kwa niaba ya wenzake kuwa watakuwa mabalozi wazuri.
Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Prof. Eliamani Sedoyeka alitangaza kuanza kwa kozi mpya takribani Saba za masomo ya shahada za Uzamili na kozi mbili za shahada za Uzamivu (PhD.) Aidha, aliwakaribisha wananchi wote kutembelea Kampasi ya IAA Dar es salaam na alitangaza kuwa muhula mwingine ni mwezi Machi na Septemba 2020.
Katika mahafali hayo Wahitimu sita walioongoza katika masomo yao ambao ni Esther Kilongola, Maimuna Kassim, Sarah Boniface, Haytham Nassor, Lucy Cassian, Neema Israel Peter, Rabia Mvungi na Salyungu Salyungu walipokea cheti na baadhi yao ngao kama pongezi kutoka IAA.
SHOW KALI YA PROF. JAY MKUTANO WA CHADEMA AWANYANYUA MBOWE, SUGU, NA LEMA