Top Stories

Halima Mdee alivyotinga kuhojiwa Bungeni, Kamati yashindwa kusema neno (+video)

on

January 22, 2019 Mbunge wa Kawe Halima Mdee alifika mbele ya Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge ikiwa ni kutekeleza agizo lililotolewa na Spika Job Ndugai ya kumtaka ahojiwe kuhusu tuhuma za kuunga mkono kauli ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) Prof. Mussa Assad kwamba Bunge ni dhaifu.

Mdee aliyeongozana na rafiki yake ambaye ni Mbunge wa Bunde Mjini Ester Bulaya aliwasili katika viwanja vya Bunge mnano saa 5 za asubuhi ambapo alianza kuhojiwa na kamati hiyo hadi majira ya saa 7 za mchana.

Mara baada ya mahojiano kumalizika Mwenyekiti wa Kamati hiyo Emmanuel Mwakasaka hakuweza kuzungumza na Waandishi wa habari kama ilivyo kawaida ya kueleza kilichojiri kwa madai kwamba hana nafasi.

“CLUB YA KWANZA MWANZA, RAIS MAGUFULI ALIICHEZA 1985”

Soma na hizi

Tupia Comments