Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru mfanyabiashara Yusuf Manji katika kesi ya kutumia dawa za kulevya baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha kosa hilo.
Katika kesi hiyo, Manji alidaiwa kati ya Februari 6 na 9 mwaka 2017 katika eneo la Upanga Sea View Ilala Dar es salaam, alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin.
Hii ni mara nyingine kwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumuachia huru Yusuf Manji kwani September 14 2017 aliachiwa huru na Mahakama hiyo kwenye kesi ya uhujumu uchumi baada ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka (DPP) kuwasilisha hati akionyesha kutokuwa na nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya Manji na wenzake.