BreakingNews

BREAKING NEWS: Kutoka Polisi jioni hii kuhusu Yusuph Manji

on

Mfanyabiashara maarufu wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Club ya soka ya Yanga Yusuph Manji ni miongoni mwa Watu 65 waliotajwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwenye orodha ya sakata la dawa za kulevya.

Manji ambaye alikwenda Polisi toka Alhamisi iliyopita, leo jioni ameonekana na Waandishi wa habari nje ya kituo cha Polisi kati Dar es salaam akichukuliwa na gari la Wagonjwa lenye namba za usajili za DFP na kuondoka nae.

Kwenye msafara huo ulioondoka gari lake aina ya Range Rover lilikuwepo pia lakini yeye alichukuliwa na gari la Wagonjwa lenye namba za usajili za DFP, muda mfupi ujao AyoTV na millardayo.com zitakuletea video fupi ikionyesha mazingira ya ilivyokua.

ULIPITWA? Yusuph Manji alivyoongea na Waandishi wa habari baada ya kutajwa kwenye orodha ya Paul Makonda… tazama kwenye hii video hapa chini

VIDEO: Yusuph Manji alivyofika kituo cha Polisi kati February 9 2017 baada ya kutajwa kwenye orodha ya Paul Makonda

BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako Millard Ayo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID NA IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo

Soma na hizi

Tupia Comments