Kamishna Mkuu UNHCR Filippo Grandi leo February 6, 2019 amemuomba radhi Rais Magufuli kufuatia Serikali ya Tanzania kukamata makontena yaliyoingizwa nchini yakiwa na nguo zinazofanana na sare za jeshi hali iliyolazimu nguo hizo kuchomwa moto, na kubainisha kuwa jambo hilo halitajirudia.
“Ilitokea kampuni moja ya Japan ilitoa msaada wa nguo kwa ajili ya wafanyakazi wetu, nguo zile kwa bahati mbaya zilikuwa zinafanana kama sare za jeshi, na tulizipokea ili tuzisambaze kwenye maeneo ambayo tunawahudumia wakimbizi, hili ni kosa, hatukupaswa kufanya hivyo na hatujawahi kufanya hivyo, lakini wakati mwingine vitu hivi vinatokea, namuomba radhi Rais na namuahidi kuwa haitatokea tena” Grandi
Rais Magufuli amempongeza Grandi kwa uungwana wake wa kuomba radhi kwa kitendo cha kuingiza nguo zinazofanana na sare za jeshi na amesema anaamini UNHCR haitarudia kufanya hivyo.
BREAKING: RAIS MAGUFULI AMPA DAWA YA BUNDI SPIKA, “TUMUOGOPE MUNGU”