Top Stories

BREAKING: Spika kufuta mshahara, malipo yote ya Tundu Lissu “anazurura duniani” (+video)

on

Spika wa Bunge Job Ndugai amesema atasimamisha mshahara na malipo yote ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kutokana na kwamba ofisi yake hadi sasa haina taarifa yoyote sahihi ya kujua Mbunge huyo yupo wapi kwa sasa.

Spika Ndugai ametoa kauli hiyo wakati akijibu muongozo wa Mbunge wa Geita Vijijini ambaye amedai Lissu hayupo hospitali, Bungeni wala Tanzania na hajulikani anafanya nini huko aliko kwa sasa na kwamba hana sababu ya kuendelea kulipwa mshahara wakati huohuo akionekana kulitukana Bunge na Serikali.

WAZIRI LUGOLA “KESI YA TUNDU LISSU IMETELEKEZWA, DEREVA WAKE AMEKIMBIA”

Soma na hizi

Tupia Comments