AyoTV

Rugemalira, Sethi wamefikishwa tena Kisutu leo, maamuzi ya Mahakama je?

on

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo July 14, 2017 imeahirisha kesi inayowakabili James Rugemalira na Harbinder Singh Sethi baada ya upande wa utetezi kusema mmoja wa watuhumiwa hao kutokuwa na afya nzuri kutokana na kusumbuliwa na uvimbe tumboni.

Wakili wa utetezi, Alex Balomi alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa mteja wake Sethi ana matatizo ya kiafya na anahitaji mtaalmu ambaye atalishughulikia tatizo lake la uvimbe tumboni lililosababisha kukosa usingizi kwa wiki nne.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali, Leornad Swai alidai nyaraka zilizowasilishwa Mahakamani hapo kuonyesha kuwa Sethi ni mgonjwa hazina usahihi na hazionyeshi zimetoka katika Hospitali gani.

Kesi imeahirishwa hadi July 22, 2017.

Adhabu itakayowakuta ambao hawakupeleka vyeti vyao ili vihakikiwe!!!

Soma na hizi

Tupia Comments