Michezo

Mo Dewji acharuka “Sijaondoka Simba na wala sijazuiwa” (video+)

on

Mfanyabiashara na Muwekezaji wa Simba SC Mo Dewji ambaye anamiliki 49% ya hisa za Simba SC kwa thamani ya Tsh Bilioni 20 leo amewataka Wapenzi wa Simba kupuuza upotoshaji unaodai ameondoka Simba na kusema bado yeye ni Muwekezaji wa Simba na ataendelea kuijenga Simba.

Mo amewataka pia Watu kupuuza upotoshaji unaodai amejiuzulu Uenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba kutokana na maelekezo y FCC na kusema hiyo sio kweli huku akisisitiza kuwa amefikia uamuzi huo kutokana na mara nyingi kutokuwa nchini.

Ayo TV & Millardayo.com imekusogezea video huu ufahamu alichozungumza Mo Dewji.

KUJIUZULU KWA MO DEWJI, EDO KUMWEMBE AMTETEA, HAJI MANARA NA MPOKI WATIA NENO

Soma na hizi

Tupia Comments