Top Stories

MO Dewji amjibu Kigwangalla “nisamehe”

on

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Mohammed Dewji amemalizana na mwanachama wa Simba, Hamisi Kigwangalla baada ya wawili hao kutupiana maneno kwenye mitandao ya kijamii yaliyokuwa yakihusisha uwekezaji wake kuelekea mfumo wa mabadiliko ndani ya klabu hiyo.

MO Dewji kupitia mitandao yake ya kijamii amesema kuwa wote wana mapenzi ya dhati na Simba, na kutumia nafasi hiyo kuomba radhi pale alipokosea na yeye kwa upande wake alipokosewa na Kigwangalla amesamehe.

”Nia njema ni tabibu, nia njema ni ibada, sote tuna mapenzi ya dhati na Simba, hata tulipokwazana ilikua katika nia njema kwenye maendeleo ya timu yetu, naomba radhi nilipokosea na mimi uliponikosea nishasamehe, tuijenge Simba pamoja sasa” MO Dewji

BWENI LA ‘MAGUFULI’ LA BUMANGI SEKONDARI LATEKETEA KWA MOTO

Soma na hizi

Tupia Comments