Michezo

MO Dewji amkaribisha Simba SC Rais wa FIFA

on

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Simba SC MO Dewji leo amefanikiwa kukutana na Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Duniani (FIFA) Gianni Infantino, MO Dewji amekutana na kujadiliana na Rais huyo, MO ame-share picha zake na Infantino katika mitandao ya kijamii.

Leo nimekutana na Gianni Infantino, Rais wa FIFA katika makao yao makuu. Kwa kweli nimefurahishwa sana, kwa dira na shauku ya kuendeleza mpira wa ushindani na wa kuvutia Afrika. Nia yao ni kuboresha maendeleo ya mpira, na najua chini ya uongozi wa Gianni mpira wa miguu kwenye bara letu utaenda next level”>>>MO Dewji

Hii sio mara ya kwanza kwa MO Dewji kutembelea timu kubwa duniani na kukutana na viongozi wa soka, aliwahi kwenda katika club ya Juventus pia lakini hajaweka wazi nini hasa amekusudia kufanya katika kukutana kwake na viongozi hao.

Soma na hizi

Tupia Comments