Michezo

MO Dewji arusha dongo “hakuna mkubwa kuliko Simba” (+video)

on

“Hii taasisi iendeshwe kwa uwazi na nidhamu ya hali ya juu, hakuna mtu mkubwa kuliko Simba, tumeikuta sisi tutakufa tutaiacha. MO ni mdogo sana kwa Simba, hatutakubali mtu kuwa mkubwa au kuwa juu ya Simba hata kama ni MO.” – MO Dewji.

“Lengo letu kuendelea kutetea ubingwa wa Ligi, kushinda kushinda vikombe, lakini hii nusu fainali sasa haipendezi tena, sitaridhika mpaka nichukue Ubingwa wa Afrika. Nimemsikia Kocha wa Al Ahly anasema amefungwa Bayern München na Simba, na Simba ndiyo ilimpa ugumu.” – Mo Dewji.

“Al Ahly ana uwezo wa kununua mchezaji wa dola mil 1 mpaka dola mil 2, sisi lazima tujipange, hivyo kuna mipango mikubwa na kamati maalum ambayo inafanyia hiyo kazi ili bajeti yetu iwe mara 4 au 5 zaidi, lengo letu kushinda Ligi ya Mabingwa Afrika.” – Mo Dewji.

“Tumeanza na Mo Simba Arena, tuna mipango mikubwa, tutakuja na program ya kujenga viwanja nane, tuwe na Academy yetu, Youth Programs, real estates ili tuweze kuingiza mapato na kushindana na Al Ahly.” – Mo Dewji.

Soma na hizi

Tupia Comments