Michezo

MO Dewji katua Uganda na kutangaza dau nono kwa Kilimanjaro Stars

on

Bilionea na muwekezaji wa Simba SC MO Dewji akiwa nchini Uganda alipokutana na wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania bara “Kilimanjaro Stars” ameahidi endapo watachukua Ubingwa wa CECAFA 2019 atawapa zawadi ya Tsh Milioni 100 na pikipiki “MO Boxer”.

“Kama Mtanzania ambaye napenda kuona nchi yangu inafanya vizuri kwenye soka nimeahidi kutoa zawadi ya Tsh100m na zawadi ya pikipiki za MO Boxer kwa wachezaji na benchi la ufundi la timu yetu ya iwapo itashinda ubingwa wa michuano ya CECAFA ambayo inafanyika hapa nchini Uganda”>>> MO Dewji
.
December 10 Kilimanjaro Stars itacheza dhidi ya Zanzibar Heroes katika mchezo wake wa pili ikiwa inaingia uwanjani na kumbukumbu mbaya ya kupoteza mchezo uliopita kwa kufungwa kwa goli 1-0 dhidi ya Harambee Stars.
VIDEO: PAMBANO LA ROUND 10: MWAKINYO VS TINAMPAY

Soma na hizi

Tupia Comments