Michezo

MO Hussein “Kila mmoja ashinde mechi zake”

on

Simba SC baada ya kumalizana na hatua ya Makundi Afrika kesho watarejea Uwanja wa Mkapa kuikabili Mtibwa Sugar katika muendelezo wa michezo ya Ligi Kuu Tanzania bara 2020/21.

Kuelekea mchezo huo nahodha msaidizi Simba SC Mohamed Hussein ameweka wazi kuwa licha ya kuulizwa sana kuhusu Ubingwa hususani Yanga mpinzani wao akiongoza Ligi akiwa kawazidi michezo na kama Simba wakishinda mechi za viporo wanaweza kukaa kileleni.

“Suala la Ubingwa naweza kusema kila mmoja ashinde mechi zake, sababu ukiangalia sana mwenzako anafanya nini focus (malengo) yako inaweza ikapotea sisi kama wachezaji target yetu kila mechi ni kupata point 3”>>> Mohamed Hussein

Yanga SC kwa anaongoza Ligi kwa kuwa na point 51 akiwa kacheza michezo 24 wakati Simba SC wakiwa nafasi ya tatu kwa kuwa na point 46 akiwa kacheza michezo 20, hivyo Yanga akiwa mbele kwa michezo minne.

Soma na hizi

Tupia Comments