Michezo

Wachezaji watano ambao kama Jose Mourinho atakuwa kocha wa Man United watapenda kuondoka …

on

Headlines za Jose Mourinho kuhusishwa kukaribia kujiunga na klabu ya Manchester United bado zinazidi kushika kasi sehemu mbalimblia, kwa wapenzi na mashabiki wa soka duniani kote kwa sasa vijiwe vyao mara nyingi mada kuu ni Louis van Gaal na Jose Mourinho. December 25 Mtu wangu wa nguvu nimekutana na list kutoka sokka.com ya wachezaji watano wa Man United ambao kama Jose Mourinho atajiunga Man United watapenda kuondoka.

5- Sergio Romero ni golikipa wa kimataifa wa Argentina na alisajiliwa na Louis van Gaal, ila kwa siku za karibuni aliwahi kusema kuwa Man United sio timu ya kiwango chake, licha ya kuwa ni golikipa wa akiba baada ya David de Gea lakini kama Mourinho akijiunga na Man United nafasi yake itakuwa finyu kwani, Mourinho anaweza kumrudisha Victor Valdes ambaye alikorofisha na Louis van Gaal.

MANCHESTER, ENGLAND - AUGUST 05: (EXCLUSIVE COVERAGE) Sergio Romero of Manchester United in action during a first team training session at Aon Training Complex on August 5, 2015 in Manchester, England. (Photo by John Peters/Man Utd via Getty Images)

Sergio Romero

4- Michael Carrick ambaye msimu uliopita alikuwa kiungo wa kati chaguo namba moja kwa Van Gaal anatajwa kupungua kasi, huenda labda kutokana na umri wake wa miaka 34 umeanza kulitupa soka mkono, hivyo kama Mourinho akiingia Man United anaweza asiendane na mfumo wake kutokana na kupungua kasi.

Michael-Carrick7

Michael Carrick aliyepitwa na mchezaji wa timu pinzani

3- Marouane Fellaini ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Ubelgiji, msimu uliopita alionesha uwezo mzuri na alikuwa ni moja kati ya nguzo muhimu katika timu, kitu ambacho ni tofauti na msimu huu amekuwa akicheza kwa taratibu au bila kasi unaweza kusema, huyu pia atashindwa kwenda na mfumo wa Mourinho.

Marouane-Fellaini7

Marouane Fellaini

2- Daley Blind alisajiliwa na Louis van Gaal mwishoni mwa dirisha la usajili la majira ya joto kwa mwaka 2014 kama kiungo mkabaji ila ameonekana akitumika katika nafasi tofauti tofauti, kama beki wa kati na beki wa kushoto, kitu ambacho kinaashiria kuwa hana namba maalum na sio aina ya mchezaji ambaye Mourinho anaweza kumtumia katika safu yake ya ulinzi.

Daley-Blind2

Daley Blind

1- Juan Mata aliondoka Chelsea January 2013 kwa sababu Jose Mourinho alikuwa hamuhitaji, licha ya kusajiliwa kwa dau nono la pound milioni 37, nyota huyo mahusiano yake mazuri na Mourinho yalizidi kuvunjika kiasi kwamba ilifikia wakati hawaongei wawili hao, kitu kilichomfanya Mata aamue kuondoka Chelsea na kujiunga na Man United.

Jose-Mourinho-v-Mata

Juan Mata

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments