Duniani

Huyu ndiyo mrembo mwenye ulemavu wa miguu na anaingiza Mamilioni kila siku !! (Pichaz&Video)

on

Kanya Sesser ni binti wa miaka 23 ambaye alizaliwa akiwa na ulemavu wa kutokuwa na miguu, lakini yeye ni moja ya wanawake wajasiri zaidi Duniani ambao wameamua kuthubutu na kufanikiwa kujiweka kwenye njia ya kujiingizia pesa nyingi kupitia masuala ya fashion.

mode

Sesser alizaliwa Thailand, familia yake ilimtenga ndani ya kipindi cha wiki moja tu tangu azaliwe na kujikuta akilelewa mikononi mwa watu baki hadi alipofikisha umri wa miaka 15 na kujiingiza katika mambo ya mitindo kupitia kuzitangaza nguo za ndani za wanawake.

mode4

Amesema hajutii kuzaliwa hivyo na kuamua kujihusisha na mitindo ambapo ameingia mkataba na makampuni makubwa kama Volcom, Nike na Rip Curl Girl… Mrembo huyu kwa siku anaingiza zaidi ya Dola 1000 ambazo ni zaidi ya Milioni mbili za Kitanzania.

mode6

Mbali na mitindo pia Sesser ni mwanariadha na sasa yupo katika maandalizi ya kushiriki mbio za walemavu zitakazofanyika Korea Kusini mwaka 2018.

mode11

Kanya Sesser akiwa na mlezi wake baada ya kutengwa na familia yake

mode7

mode2

juu

 

lov

Kanya Sesser akiwa na mpenzi wake Brian Waters

Stori yake iko kwenye hiki kipande cha video pia..

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa, muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>YouTUBE

Tupia Comments