Iwapo itathibitishwa, mkataba wake utavunja rekodi ya dunia ya Cristiano Ronaldo.
Nyota wa soka wa Misri, Mohamed Salah, ameripotiwa kupewa karibu dola milioni 80 ili kumjaribu kuondoka Liverpool kwa misimu miwili nchini Saudia Arabia.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 yuko katika msimu wake wa mwisho katika klabu hiyo ya Uingereza ikiwa hatasaini mkataba mpya na timu hiyo.
Lakini mvuto wa mshahara ambao unaripotiwa kuwa karibu mara mbili ya ule anaopata akiwa Liverpool itakuwa vigumu kuupinga.
Fowadi huyo ni mmoja wa wanasoka watatu wanaoaminika kuwa wanafikiria kuondoka The Reds, huku dirisha la uhamisho likiwa linaendelea.
Kuna ripoti kwenye vyombo kadhaa vya habari kuwa Salah yuko kwenye mazungumzo mazito na klabu ya Al-Hilal ya Saudia ili kufanikisha uhamisho wake kwenye timu hiyo.
Kuondoka kunakotarajiwa katika majira ya joto ya Neymar wa Brazil kunamaanisha kwamba klabu itakuwa na nafasi katika kikosi chao kusajili mchezaji mwingine wa ng’ambo.
Pia kuna ripoti zinazosema Al-Hilal yuko kwenye mazungumzo na uongozi wa Liverpool kununua miezi sita iliyobaki ya kandarasi ya Salah.
Hii ingewezesha uhamisho wake wakati wa dirisha la uhamisho wa majira ya baridi linaloendelea