Halmashauri ya Wilaya ya Monduli imesaini mkataba wa kihistoria wa ukarabati wa skimu za umwagiliaji katika Bonde la Mto wa Mbu, hatua inayolenga kuboresha kilimo cha umwagiliaji na kupunguza athari za mafuriko.
Katika hafla hiyo, Mbunge wa Jimbo la Monduli, Fred Lowasa, amesema kuwa mradi huu uliogarimu zaidi ya bilioni 17 unalenga kuimarisha mifereji ya umwagiliaji, ambayo imekuwa changamoto kwa miaka mingi kutokana na uchakavu na mafuriko ya mara kwa mara.
Aidha ameongoza kuwa serikali inafanya kazi kubwa kupitia Tume ya Umwagiliaji. Katika kuwezesha sekta hiyo kwa kutoa fedha zinazohitajika ili kuhakikisha kilimo cha umwagiliaji kinasaidia wakulima kwa uhakika wa msimu bila kusubiri mvua.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Festo Kiswaga,ambae ndie mgeni rasmi katika fukio hilo amesema kuwa serikali imejipanga kuhakikisha kilimo cha Tanzania hakitegemei mvua pekee, bali kinatumia umwagiliaji wa uhakika huku serikali ikihakikisha kupitia kilimo cha umwagiliaji njaa inakuwa historia. kudhibiti mafuriko ambayo yamekuwa yakisababisha hasara kwa wananchi.
Naye Aretasi Protasi kutoka Ofisi ya Umwagiliaji, alieleza kuwa mradi wa Bilioni 17 ni moja kati ya skimu 10 kati ya 17 zinazofanyiwa maboresho katika Bonde la Mto wa Mbu. Huku moja ya changamoto kubwa ikiwa ni mifereji kufukiwa na mafuriko, pamoja na wanyamapori na mifugo kuingia kwenye skimu
Nao wakulima watakao nufaika na mradi huo wakaishukuru serikali huku wakieleza changamoto zilizokuwa zinawakabili pamoja na manufaa watakayi yapata baada ya kukamilija kwa mradi huo.
Serikali inatarajia kwamba mradi huu utakapokamilika, utachangia kuboresha shughuli za kiuchumi, hasa katika sekta za kilimo na ufugaji kwa wananchi wa Monduli na Mto wa Mbu huku kampuni ya Jandu plumbers , ambayo imepewa zabuni ya kutekeleza mradi huo kuaswa kukamilisha mradi huo kwa viwango na muda ulio pangwa.