Ukubwa wa hit kadhaa kutoka kwa Young Killer ‘Msodoki’ umefanikishwa kwa asilimia kubwa sana na Producer Mona Gangstar kutoka Classic Sound ambaye amefanya hit kadhaa za Young Killer.
Kwenye mahojiano na milladayo.com hivi karibuni Mona Gangstar alikubali kutoa ya moyoni ambayo pengine awali yalikua yakinukuliwa tofauti na yeye alivyo baina yake na msanii aliyekuwa akimsimamia kazi zake Young Killer.
Swali la kwanza lilikuwa ni kutaka kujua kwa sasa yeye na Young Killer wako vipi toka walipositisha mkataba wao katikati ya mwaka 2014 ambapo alijibu kuwa wako vizuri ingawa wanaonana barabarani tu na kupishana.
Kuhusu kama yuko tayari kufanya kazi tena na Young Killer,Producer Mona Gangstar amesema kuwa yupo tayari kama Young Killer ataweza kumudu gharama za kurekodi yuko tayari kufanya nae kazi.
Swali lingine lilikuwa kama ikitokea Young Killer anarudi rasmi na kutaka kufanya nae kazi kama zamani kwake itakuaje ambapo alijibu kuwa akikamilisha taratibu zake inawezekana ila kwa sasa hana msanii na kuna taratibu zake anaziweka sawa kwanza.
Kauli yake nyingine alisema kuwa kama ataona bado ana nguvu (impact) wanaweza kufanya tena kazi,lakini kama hana nguvu hawawezi tena kufanya kazi kwa sababu hawezi kufanya biashara ambayo haina faida.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyezahapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahaukusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTVikufikie.