Habari za Mastaa

Ni FurahiDay na Monica anaileta kwako hii mpya; ‘Just Right For Me’ feat. Lil Wayne – (Video)!

on

Mara ya mwisho umemsikia Monica ilikuwa ni lini? Imepita muda kidogo toka msanii wa muziki wa R&B kutoka Marekani, Monica Brown azikamate headlines za burudani, na ninajua nina watu wangu ambao ni mashabiki wakubwa wa muziki wa Monica, kama wewe ni mmoja wao basi hii good news ikuguse popote pale ulipo!

Monica anategemea kudondosha Album yake mpya iliyopewa jina Code Red tarehe 18 December 2015… lakini kwa sasa msanii huyo mkongwe wa muziki wa R&B anaisogeza kwako single mpya kutoka kwenye Album yake, Just Right For Me na video yake ipo hewani tayari.

MONICA2

Ndani ya video hii, Lil Wayne ameshirikisha huku Director wa video hiyo wakiwa The Rite Brothers, na kwenye interview ya uzinduzi wa video yake mpya Monica alikuwa na haya ya kusema…

>>> Nina mategemeo makubwa na hii video mpya, kwa sababu imepita muda mrefu toka niwape mashabiki wangu flava kali ya original R&B na niliamua kumshirikisha Lil Wayne kwa sababu nina vibe kubwa na Wayne na amekuwa mstari wa mbele kunisaidia baadhi ya vitu kwenye video hii. Natumaini mashabiki wataipenda“. <<< Monica Brown.

MONICA3

Tarehe 12 November 2015, Monica atazindua tour yake kwa ajili ya kuisambaza Album yake mpya ‘Code Red’… inawezekana mdundo huu umeshakufikia lakini kama hujafanikiwa kukutana na video hiyo mpaka sasa, karibu uicheki video hiyo hapa chini kwa kubonyeza play.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments