Hii taarifa tayari imeripotiwa mitandaoni na kwenye vyombo vingi vya habari kutoka Mkoa wa Morogoro ambapo inahusu kutolewa kwa hukumu ya Sheikh Issa Ponda ambaye ameachiwa huru baada ya kukutwa hana hatia.
Sheikh Issa Ponda alishtakiwa kwa makosa matatu ikiwemo kukiuka amri ya Mahakama kufanya mkusanyiko pamoja na kutoa maneno ya uchochezi… Mawakili wa Sheikh Issa Ponda wamesema waliamini haki itatendeka japo imechelewa.
Baada ya hukumu hiyo, Sheikh Ponda aliondoka kuelekea kwenye Msikiti wa ‘MUNGU Mmoja Dini Moja‘ uliopo Morogoro kwa ajili ya kuongea na waumini wake.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na MillardAyo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE