Klabu ya Mchezo wa Polo ya Palmeraie imeshinda mashindano maalum yaliyoandaliwa na Mfalme wa Morocco Mohammed wa Sita yakidumu kwa siku tano kuanzia Novemba 14-19 katika viwanja vya Souissi huko Rabat.
Mabingwa hao walishinda mchezo wa fainali dhidi ya Garde Royale kwa pointi 6-5 katika mashindano haya yaliyokuwa yanaandaliwa kwa mwaka wake wa pili
Mshindi wa tatu kwenye mashindano hayo alikua klabu ya Jnan Amar De Marrakech akishinda dhidi ya Ecole Royale De Cavalerie kwa pointi 11-4 katika mchezo uliopigwa Jumamosi.
Kwenye Hatua ya nusu fainali Garde Royale walishinda dhidi ya Ecole Royale na mabingwa Palmeraie walishinda mchezo wa nusu fainali dhidi ya Jnan Amar.
Katika Hatua ya fainali Rais wa shirikisho la Michezo ya Majini yaani Equestrian Sports Moulay Abdellah Alaoui alikabidhi kombe kwa nahodha wa timu mabingwa
Hii ni ishara nyingine ya ushirikiano wa kutosha inayopata sekta ya michezo Morocco toka kwa serikali ya taifa hilo chini ya mfalme wake Mohamed wa sita.