Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) Kushirikiana na Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu na Manispaa ya Morogoro wamefanya usafi katika chanzo cha maji Vituli kata ya Bingwa Manispaa ya Morogoro na kubaini kuwepo kwa baadhi ya watu kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya mita sitini kutoka chanzo cha maji na Mto mgolole
Hali hiyo imebainika baada ya Mamlaka hizo kufika katika mto huo kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi kuacha kutopa taka za plastiki katika vyanzo vya maji na kukuta baadhi yao wakifanya uharibifu huo ambapo afisa maendeleo ya jamii Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu Yuliani Mizola anatumia nafasi hiyo kutoa elimu kwa wananchi kutojenga vyoo karibu na chanzo cha mto kwani kunaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa ikiwemo Kipindupindu.
Kwa upande wake msimazi wa mazingira MORUWASA Mhandisi Rashid Bumalwa wamesema kutokana na uchafunzi huo wamekua wakitumia gharama kubwa kutibu maji.
Amesema kama.mamlaka inawakumbusha wananchi kuendelea kutunza na kuhifadhi vyanzo vya maji ili kuepukana na changamoto ya ukosefu wa maji pindi vyanzo hivyo vitakavyokauka.
Naye afisa mazingira Manispaa ya Morogoro Fatma Juma amesema licha ya kufanya usafi katika vyanzo vya maji lakini wamekua wakitoa elimu kwa wananchi kufanya usafi hadi katika makazi yao hivyo mpango kutoa elimu zaidi kwa wakazi wanaoishi karibu na yanzo vya maji ili kuona umuhimu wa vyanzo hivyo.
Amesema sheria ya Mazingira inakataza kufanya shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo,ufugaji,uchimbaji madini na ujenzi wa nyumba ndani ya mita sitini kutoka kwenye chanzo cha maji.