Club ya Al Ahly imetangaza kuwa Kocha wao Mkuu Raia wa Afrika Kusini Pitso Mosimane (57) ameomba kuondoka katika club hiyo kwa kile alichoeleza kuwa mafanikio aliyoyapa hivyo anaomba kwenda kutafuta changamoto mpya.
Mosimane alijiunga na Al Ahly 2020 akitokea Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini na kufanikiwa na kufanikiwa kuiwezesha Al Ahly kucheza fainali tatu mfululizo za Ligi ya Mabingwa Afrika huku akitwaa taji mara mbili mfululizo kati ya hizo fainali tatu.
Tetesi zinadai kuwa kwakuwa Mosimane kaomba kuondoka Al Ahly huenda akawa anatazamia kutangazwa kuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Misri, nafasi ambayo alihusishwa nayo kabla hata Kocha Carlos Queiroz hajapewa kazi na kutimuliwa hivi karibuni.