Top Stories

Moto tena Kariakoo, Hoteli yaungua kijana anaesambaza gesi asimulia “Gesi imelipuka”?

on

NI July 23, 2021 ambapo Hotel ya Rungwe Palace iliyopo Mtaa wa Livingstone Kariakoo imewaka moto ambao umezuka kuanzia ghorofa ya sita, Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na Wananchi wamefanikiwa kuuzima moto huo.

‘Mimi nilileta Gesi hapa mimi ni msambazaji sasa baada ya kuondoka kurudi ofisini nikapigiwa simu kwamba jengo limeanza kuungua nikawauliza chanzo ni nini wakaniambia ni Umeme ilibidi nirudi basi kufika hapa nikakuta moto unawaka,basi ndipo jitihada zikaendelea wakapigiwa simu vyombo vya usalama  pamoja na Zimamoto’-Shuhuda

Tulifika eneo hili la tukio na tulikutana moto unawaka floor ya sita na tulipambana kuzima moto huo ambalo ulkuwa unawaka katika chumba chao cha Store, majira ya saa nane tulifanikiwa kuuzima moto huu na tulifanikiwa kuwaokoa watu watano lakini katika watu watano hao wawili ndio waliokuwa wameathirika mmoja alikatwa na kioo na mwingine alikuwa ameathirika na moshi kwasababu alikuwa katika floor ya tano na tulifanikiwa kupambana na kuingia ndani kisha kumtoa nje’- Zimamoto

VILIO KARIAKOO: MFANYABISHARA ASHINDWA KUJIZUIA “NIACHENI, ONDOKENI”

Soma na hizi

Tupia Comments