Takriban watoto 17 waliuawa katika moto uliozuka katika shule ya Kiislamu kaskazini-magharibi mwa Nigeria, shirika la kukabiliana na dharura la nchi hiyo lilisema, wakati mamlaka ilipoanzisha uchunguzi kuhusu chanzo siku ya Alhamisi.
Shirika la Kitaifa la Usimamizi wa Dharura lilisema katika taarifa kwamba takriban watoto 100 walikuwa shuleni wakati moto huo ulipozuka siku ya Jumatano katika wilaya ya Kaura Namda katika jimbo la Zamfara.
Watoto kumi na saba walijeruhiwa vibaya na walikuwa wakitibiwa katika hospitali tofauti.
Haikuweza kufahamika mara moja kilichosababisha moto huo. Matokeo ya awali, hata hivyo, yanaonyesha kuwa moto huo ulisababishwa na mrundikano wa vijiti vinavyotumika kwa usafi wa kinywa, maarufu kama “kara,” ambavyo vilikusanywa karibu na shule hiyo, shirika hilo lilisema