Tangu mwaka 2015 umeanza tumesikia stori kadhaa za Ajali ya moto ikiwemo ile ya familia yenye watu sita wakiwa wamefariki ndani ya nyumbani chanzo kilisemakana ni itilafu ya Umeme, sasa hapa nakusogezea stori nyingine ya kusikitisha ambapo usiku wa kuamkia leo kumetokea ajali ya moto ilyouwa familia ya watu 9 wakiwa ndani ya nyumba maeneo Buguruni Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Katibu wa mtaa Amina Kichalala….’Mimi niliamshwa usiku na mume wangu akatuambia kwa jirani kuna moto ilikuwa n majira ya saa tisa usiku mara tunasikia sauti zao wanasema tuwasaidie moto ulikuwa ni mkubwa sana watu wakaanza kurusha mawe, wamejitahidi lakini moto ukawa mkubwa mpaka mida ya saa kumi na moja kasoro ndio zijaka fire kuuzima huo moto na kutoa miili ya watu tisa wakiwa washamefariki katika ajali hiyo ya moto’ – Amina
‘Sauti iliyosikika wakati tukio hilo la ajali ya moto ilikuwa ni ya msichana mdogo anaitwa Aisha yuko kama darasa la saba mtoto wa huyo Baba, katika hiyo nyumba alikuwa anaishi Mama Habilai, Mohamed, Ashlafu,Aisha na Bibi yao asiyejiweza kwasababu uwa wanamtoa kumpeleka hospitali na wageni kutoka Oman walioingia jana nao wamefariki’ – Amina
‘Majirani walifanya juhudi za kuuzima moto huo lakini hakuna kilichowezekana kwasababu moto ulikuwa ni mkubwa sana, uamuzi uliofuata ile miili 9 ya ndugu zetu imepelekwa muhimbili kuoshwa na kuzikwa katika makaburi ya Kisutu Dar es Salaam‘ -Amina
Unaweza uka bonyeza play kumsikiliza shuhuda wa tukio hilo la Ajali ya moto
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos