Michezo

Mourinho hali tete atupwa nje ya FA Cup na Tottenham yake

on

Club ya Tottenham Hotspurs wameaga michuano ya FA Cup baada ya kuondolewa kwa mikwaju ya penati 3-2 dhidi ya Norwich City kutokana na game hiyo kwenda dakika 120 kumalizika sare ya kufungana moja moja kama ilivyokuwa katika mchezo wa kwanza.

Jose Mourinho akiwa na kikosi chake cha Tottenham amekuwa na wakati mgumu kutokana na timu yake kuondolewa mapema, ushindi huo wa Norwich unamfanya acheze na mshindi wa mechi ya Derby County dhidi ya Man United.

Michezo ya robo fainali ya michuano hiyo inatarajiwa kuchezwa kati ya March 20 na 22, timu zilizofu kucheza hatua ya robo fainali ni Man City, Leicester, Norwich, Arsenal, Sheffield United, Newcasle United na Chelsea.

VIDEO: “KAMA UKITAKA UPEPO PANDA BAJAJ, KAMA UKITAKA SOKA PENDA YANGA”-MBOTO

Soma na hizi

Tupia Comments