Ad

Michezo

Hii ndio sababu iliyomfanya Jose Mourinho akiri kushindwa kumaliza Top Four …

on

December 5 siku ya Jumamosi haikuwa nzuri kwa mashabiki wa klabu ya Chelsea baada ya kupata kipigo cha goli 1-0 kutoka klabu ya Bournemouth. Chelsea ambayo ilikuwa ikicheza mchezo wa 15 ilishindwa kutamba na badala yake imefikisha jumla ya mechi 8 ilizofungwa.

Baada ya matokeo hayo, kocha wa klabu hiyo Jose Mourinho, amekiri itakuwa ni vigumu kwa sasa kumaliza ligi akiwa kwenye nafasi 4 za juu kutokana na aina ya matokeo wanayoyapata.

Jose-Mourinho-during-Chelseas-Champions-League-match-against-Porto

“Lengo letu ni kumaliza katika nne bora, kabla ya mechi hii, kulikuwa na msingi kufikiria kuwa tulikuwa na uwezo wa kujitoa katika hali hii lakini sasa labda, itatubidi kufikiria kuhusu sita bora. Nina wasiwasi bila shaka. Lakini hakuna uwezekano kwamba mwishoni mwa msimu Chelsea itakuwa ikipigana kuzuia kushushwa daraja” >>> Mourinho

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments