Michezo

Baada ya kupewa adhabu na FA, Jose Mourinho kaamua maamuzi haya…

on

Kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho ambaye yupo katika wakati mgumu kutokana na mwenendo mbovu wa timu yake. Mourinho ambaye amepigwa faini ya pound 50000 na kufungiwa mchezo mmoja kutokaa katika benchi la timu hiyo kufuatia kauli aliyoitoa kwa muamuzi kuwa aliogopa kuwapa penati.

Mourinho alipewa adhabu hiyo baada ya kutenda kosa la kumshambulia kwa maneno refa wa mechi ya Chelsea dhidi ya Southampton, mechi ambayo ilimalizika kwa Chelsea kupoteza kwa goli 3-1. Hata hivyo kocha huyo wa Chelsea alimshambulia kwa maneno refa Robert Madley hivyo FA waliamua kumuadhibu.

jose mourinho

October 16 Mourinho amethibitisha kukata rufaa kufuatia adhabu aliyopewa na shirikisho la mpira wa miguu Uingereza FA, kwani anaamini hakufanyiwa haki katika maamuzi ambayo yamefanywa na FA. Hata hivyo Mourinho ni kocha ambaye hapendi kufungwa na kama ikitokea timu yake ikafungwa basi hutoa kauli tofauti tofauti.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.

Tupia Comments