Michezo

Mourinho kapigwa stop moja… alafu na milioni 160 zinamtoka

on

Chama cha soka England (FA) kimempa kocha wa Chelsea Jose Mourinho adhabu kutokana na utovu wa nidhamu ambapo anatakiwa kulipa faini ya dola 77,000 ambazo kibongobongo ni zaidi ya milioni 160 pamoja na kufungiwa mechi moja huku FA wakiangalia mwenendo wake.

Meneja huyu wa Chelsea alimshambulia kwa maneno mwamuzi Robert Madley aliyechezesha mechi ya Chelsea vs Southampton iliyomalizika kwa 1- 3 na ikamfanya Mourinho akasirishwe na Refa Madley kutoipa timu yake penati na kudai Waamuzi wanaogopa kutoa uamuzi kwa timu yake.

Hii kauli ndio ikawafanya FA wamfungulie Mashitaka ya utovu wa nidhamu wakidai kauli za Mourinho zinazochochea vurugu.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments