Michezo

Alichosema Mourinho kuhusu kuwasajili aidha Falcao, Zlatan au Cavani

on

2w650c0.bild_Jose Mourinho ametoa ishara kwamba klabu yake ya Chelsea inaweza kutuma ofa ya kumsajili mshambuliaji wa kikolombia Radamel Falcao mara tu dirisha la usajili litakapofunguliwa.

Meneja huyo wa Chelsea hakuonyesha kuficha matamanio yake ya kumleta mshambuliaji huyo wa Colombia darajani – Falcao ambaye kwa sasa ni majeruhi wa goti – ameripotiwa kwamba anataka kuondoka kwenye ligi kuu ya Ufaransa kutokana na kutokuwepo kwa ushindani kwenye ligi hiyo.

Katika mahojiano na Canal Football Club, Mourinho aliondoa uwezekano wa klabu yake kuwasajili washambuliaji wa PSG  Zlatan Ibrahimovic na Edinson Cavani, akisisitiza ni ‘haiwezakani’ kuwasajili wachezaji hao.

Alisema: ‘Nina timu, lakini sina mshambuliaji. Falcao hana timu pale. Mchezaji kama yeye hawezi kuwa anacheza mbele ya mashabiki 3,000. Monaco ni klabu ya kumalizia soka, hampafai pale kwa sasa.”

Falcao, 28, alijiunga na Monaco kwa ada ya £50million kutoka Atletico Madrid kipindi cha kiangazi kilichopita.

 

Tupia Comments