Michezo

Moyes, Diop na Josh waugua Corona

on

Club ya West Ham United imethibitisha kuwa kocha wao David Moyes, beki wao Issa Diop na kiungo Josh Cullen wamepata maambukizi ya virusi vya Corona.

Taarifa hizo zimetoka muda mchache kabla ya mchezo wa Carabao Cup dhidi ya Hull City, hivyo Diop, Moyes na Josh Cullen wakaondolewa mapema katika list ya watakaoshiriki.

Kocha msaidizi wa West Ham United Alan Irvine ndio alikiongoza kikosi cha West Ham United katika mchezo wa round ya tatu wa Carabao dhidi ya Hull City na West Ham kupata ushindi wa magoli 5-1.

Soma na hizi

Tupia Comments