Mix

Trafiki Dar es salaam aagizwa na Boss wake kulipa faini aliyomtoza mwenye Benz

on

Jana January 25 2017 kuna comment ambayo ilikua inasambaa sana kwenye Whatsapp ikionyesha post ya Facebook ya Mtanzania ambaye amepigwa faini na Askari wa usalama barabarani (Trafiki) kwa kosa la Ubovu wa gari lake.

Post yenyewe ya Mlalamikaji akiwa kaambatanisha picha za sehemu ya gari yenye kutu ilisemaJamani nimepigwa cheti at gari ni mbovu, hii kweli ni sahihi?

Pamoja na hiyo post kuna Comment ya Facebook ikionyesha account yenye jina la Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mohammed Mpinga ikiwa imetoa comment kwa kusemanimefatilia leo asubuhi TAZARA na kubaini kwamba hakustahili kosa la ubovu wa rangi au kutu inayoonekana, nimeelekeza askari huyo alipe mwenyewe hiyo faini na kupewa onyo kali

Wengi wanataka kujua kama ni kweli hiyo Account ya Facebook ni ya Kamanda Mpinga? na ni kweli alijibu hivyo? ni baadhi ya maswali watu waliyonayo ambapo millardayo.com na AyoTV zimempata Kamanda Mpinga ambaye amesemaHiyo ilikua ni kweli, account na Facebook comment ni mimi nimetoa


.

millardayo.com na AyoTV zitamtafuta Kamanda Mpinga zaidi kujua ni njia gani wengine wanaoamini wameonewa kwenye kulipa faini zisizostahili wanaweza kufikisha malalamiko yao kama hivi.

UKO TANZANIA NA GARI LAKO LINA TINTED? kuna hivi vitu vitano unatakiwa kuvijua kuanzia sasa, bonyeza play kwenye hii video hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments